Showing posts with label michezo. Show all posts
Showing posts with label michezo. Show all posts

Monday, 2 November 2015

Motorola Launches DROID Turbo 2 And It Just Won’t Break


motorola-unbreakable-phone-1
It doesn’t matter how advanced or smart your smartphone is if it gets shattered each time it falls! The flaw isn’t fixated to Apple iPhones, which if you remember would bend inside your pockets, but to almost all the phones (except vintage Nokia) that would easily break.
Motorola has, however, come up with its own hulk version of a smartphone that just won’t break. Motorola DROID Turbo 2 is the phone which won’t bother you with the unnecessary care-taking measures while using. The DROID Turbo 2 runs on the USP of a shatterproof display along with several upgrades and is a strong contender for the people’s choice.The Turbo2 display has a five-layered structure that absorb shocks keeping your smartphone’s screen intact, claims Motorola. Also, the display is little elastic rather than being rigid to incorporate up to a certain amount force.
The Motorola DROID Turnbo 2 has a 5.4-inch Quad HD (2560 x 1440) display which comes with a four-year warranty against shattering and cracking.
After Motorola showcased its phone’s sturdiness against iPhone in an advertisement, the skeptics at CNN performed some of their own tests to check the claims of the perfect phone for the imperfect people.
Watch the official “shatterproof display” ad for DROID Turbo 2 by Motorola.

Also, watch the experiment by CNN.

+

Monday, 2 March 2015

CHELSEA YATWAA UBINGWA WA CAPITAL ONE CUP

Kikosi cha timu ya Chelsea kikiongozwa na kocha wao, Jose Mourinho baada ya kutangazwa mabingwa wa Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup 2014/15 usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Wembley kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tottenham.
Mourinho akiwa anakatiza mapambo maalum katika sherehe za kutwaa kombe hilo.
Shangwe zaidi kwa wachezaji wa Chelsea.
Mourinho akijinafasi na wachezaji wake.
Kapteni wa timu ya Chelsea, John Terry (katikati) akiwa amenyanyua kombe.
Mourinho (katikati) akiwa na kombe.
Wakishangilia ni wchezaji wa Chelsea, Cesc Fabregas (kushoto), Cesar Azpilicueta (katikati) na Diego Costa (kulia).
Diego Costa, John Terry na Didier Drogba wakiendelea na shangwe.
Mchezaji wa Chelsea, Diego Costa (kulia) akimtoka beki wa Tottenham.
Wachezaji wa Tottenham wakiwa hoi baada ya kipigo kutoka kwa Chelsea.
CHELSEA imetwaa ubingwa wa Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup usiku wa leo Uwanja wa Wembley kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tottenham.
Kombe hili ni la kwanza kwa kocha Mourinho tangu ajiunge kwa mara nyingine klabuni hapo mwaka 2013 akitokea nchini Hispania alikokuwa akiifundisha miamba ya soka nchini humo Real Madrid.
Tottenham (4-2-3-1): Lloris 6; Walker 5.5, Dier 5.5, Vertonghen 6, Rose 5.5; Bentaleb 5, Mason 5.5 (Lamela 71 6); Chadli 5.5 (Soldado 80), Eriksen 6.5, Townsend 5.5 (Dembele 62 6); Kane 5.
Subs not used: Vorm, Davies, Fazio, Stambouli,
Booked: Dier, Bentaleb
Manager: Mauricio Pochettino 5
Chelsea (4-3-3): Cech 7; Ivanovic 7, Cahill 7.5, Terry 8.5, Azpilicueta 7; Ramires 6.5, Zouma 6; Hazard 7.5, Fabregas 7.5 (Oscar 88), Willian 7 (Cuadrado 76); Diego Costa 8 (Drogba 90).
Subs not used: Courtois, Filipe Luis, Ake, Remy.
Booked: Cahill, Cuadrado, Willian
Manager: Jose Mourinho 7.5
Referee: Anthony Taylor 7
MOTM: Terry
Attendance: 89,297
+

Tuesday, 30 December 2014

SIMBA YAFUKUZA MAKOCHA



Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Mzambia, Patrick Phiri.
Aliyekuwa Kocha msaidizi, Selemani Matola (kushoto) akifuatilia mazoezi.
Klabu ya Simba imewafukuza kazi Kocha Patrick Phiri raia wa Zambia na msaidizi wake Selemani Matola kutokana na matokeo mabaya ya timu.
+

Monday, 29 December 2014

Makipa wanaolipwa zaidi: Casillas afunika ulaya

 
 
Soka ni mchezo unaopendwa sana ulimwenguni na wachezaji wengi wa mchezo huo kwenye ligi mbalimbali za Ulaya wamekuwa wakivuna fedha nyingi kutoka na mchezo huo.
Wachezaji wanaolipwa fedha nyingi ni wale wanaocheza nafasi za ushambuliaji au viungo washambuliaji. Kwa sababu Lionel Messi analipwa na klabu yake ya Barcelona Pauni 30 milioni kwa mwaka, Cristiano Ronaldo analipwa na Real Madrid Pauni 25.7 milioni kwa mwaka, Gareth Bale analipwa na Real Madrid Pauni 20.7 milioni, Neymar analipwa na klabu yake ya Barcelona Pauni 17.1 milioni kwa mwaka, Sergio Aguero analipwa na Manchester City Pauni 16.3 milioni kwa mwaka, Wayne Rooney analipwa na Manchester United Pauni 15.4 milioni kwa mwaka, Zlatan Ibrahimovic analipwa na PSG Pauni15 milioni kwa mwaka na Yaya Toure analipwa na Manchester City Pauni14.2 milioni.
Hata hivyo, hali ni tofauti kwa makipa kwani huwa hawalipwi fedha nyingi kwa mwaka kama ambavyo wanalipwa washambuliaji. Wafuatao ni makipa wanaoongoza kwa kulipwa fedha nyingi kuliko makipa wengine:
1-Iker Casillas
Kipa Iker Cassilas wa Real Madrid ndiye anayeshika nafasi ya kwanza kwa kulipwa mshahara mkubwa duniani kwani kwa mwaka analipwa Pauni 6.3 milioni.
2-Manuel Neuer
Kipa wa Bayern Munich, Manuel Neuer ndiye anayeshika nafasi ya pili kwa makipa wanaolipwa zaidi kwa sababu analipwa Pauni 5.6 milioni.
3-Petr Cech
Cech ni kati ya makipa bora katika Ligi Kuu ya England. Petr Cech analipwa na Chelsea mshahara wa Pauni 5.2 milioni kwa mwaka.
4-Joe Hart
Kipa wa Manchester City, Joe Hart ambaye amekuwa na misimu mizuri analipwa mshahara wa Pauni 4.68 milioni kwa mwaka.
5-Pepe Reina
 Kipa Pepe Reina wa Bayern Munich anashika nafasi ya tano kwa makipa wanaolipwa zaidi. Kiasi anacholipwa hivi sasa na Bayern ni Pauni 4.16 milioni kwa mwaka.
6-David De Gea
Kipa wa Manchester United, David De Gea hivi sasa yupo katika kiwango cha juu hivi sasa, klabu yake inamlipa mshahara wa Pauni 3.64 milioni kwa mwaka.
7-Hugo lloris
Kipa wa Tottenham, Hugo Lloris hivi sasa analipwa na klabu hiyo mshahara wa Pauni 3.59 milioni kwa mwaka.
8- Gianluigi Buffon
Kipa mzoefu wa Juventus, Gianluigi ‘Gigi’ Buffon anashika nafasi ya nane katika makipa wanaolipwa mishahara mikubwa. Buffon analipwa mshahara wa Pauni 3.17 milioni kwa mwaka.
9-Claudio Bravo
Kipa huyu wa klabu ya Barcelona analipwa na klabu hiyo Pauni 2.77 milioni kwa mwaka.
10-Salvatore Sirigu
Kipa anayefunga orodha ya makipa wanaolipwa fedha nyingi ni kipa wa Paris Saint Germain, Salvatore Sirigu. Kipa huyu analipwa mshahara wa Pauni 2.6 milioni kwa mwaka.
+

Sunday, 28 December 2014

Cristiano Ronaldo akiwa kwenye vazi la kanzu huko Dubai


 
 
Cristiano Ronaldo akiwa kwenye mavazi ya kiislam akipiga picha na mashabiki huko Dubai.Mchezaji nyota wa mpira wa miguu anaeichezea timu kubwa tajiri duniani Real Madrid alionekana na kupigwa picha na mapaparazi kwenye matembezi yake binafsi Dubai akiwa amevalia mavazi ya Kiislam na yaliompendeza sana.Cristiano Ronaldo ambaye yeye si Muislam lakini alipendezwa na uvaaji huo kwani alisema aliona watu wengi waishio Dubai ndio vazi lao kuu na kwanini yeye asiwe miongoni mwa waliovaa vazi hilo. Pia hakuwahi kuvaa vazi la dini hiyo alionelea avae kwa ishara ya kuiheshimu dini hiyo na kuona sio kitu kibaya kuwa miongoni kwao kimavazi.
 
Cristiano Ronaldo akiwa kwenye vazi jingine la kiislamu huko DubaiMchezaji huyo alikuwa Dubai wiki iliyopita kwenye mapumziko yake binafsi mbali na shughuli za kimpira. Alienda kutembea huko kabla ya wiki ya sikukuu za christimas. Alionekana ni mwenye kufurahishwa na mandhali ya mji huo pia utamaduni wao wa chakula pia kimavazi ndio mana nae alipendezwa kuvaa kama wao. 
Vazi lingine alilovaa mchezaji Cristiano Ronaldo akiwa kwenye matembezi yake binafsi Dubai.Mchezaji huyo alikaa Dubai kwa siku nne wiki ilopita na baadae aliondoka kurejea Hispania ambapo alijiunga na wachezaji wenzake kwenye kambi ya maandalizi ya mechi zilizoendelea katika ligi ya ichi hiyo anakochezea
+

YANGA VS AZAM NGOMA DROO,

Mshambuliaji wa Yanga, Danny Mrwanda (kulia) akijaribu kumtoka beki wa Azam FC.
Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima akiwa kazini wakati wa mechi ya leo dhidi ya Azam FC.
TIMU za Yanga na Azam FC leo zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya bao 2-2 kwenye mtanange wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Azam yamewekwa kimiani na Didier Kavumbagu katika dakika ya 5 huku la pili likifungwa na John Bocco, dakika ya 65. Mabao ya Yanga ymefungwa na Amissi Tambwe katika dakika ya 7 pamoja na Simon Msuva dakika ya 51.
+

FULL TIME: TOTTENHAM HOTSPUR 0-0 MANCHESTER UNITED

Robin van Persie wa Manchester United akijaribu kufunga bao lililookolewa na kipa Hugo Lloris wa Spurs.
Patashika wakati wa mtanange wa leo.
Mchezaji wa Tottenham, Nacer Chadi (kulia) akiruka juu kuwania mpira na Antonio Valencia wa Manchester United.
TIMU za Tottenham Hotspur na Manchester United zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka suluhu katika mechi yao ya Ligi Kuu England iliyomalizika kwenye Uwanja wa White Hart Lane hivi punde.
VIKOSI VYA LEO
Tottenham: Lloris, Chiriches, Fazio, Vertonghen, Davies, Mason, Stambouli; Chadli, Eriksen, Townsend, Kane
Waliokuwa benchi: Vorm, Dier, Walker, Lamela, Dembele, Paulinho, Soldado
Manchester United: De Gea, Jones, McNair, Evans, Valencia, Carrick, Rooney, Mata, Young, Van Persie, Falcao
Waliokuwa benchi: Lindegaard, Rafael, Smalling, Shaw, Fletcher, A.Pereira, Wilson
+

Wednesday, 17 December 2014

Maximo anatia huruma, awaaga wachezaji kwa majonzi

Kocha Mkuu wa Yanga, Mbrazili, Marcio Maximo. Na Waandishi Wetu
AKIWA na uso wa huzuni, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mbrazili, Marcio Maximo, jana alifika kwenye mazoezi ya timu hiyo asubuhi na kuwaaga wachezaji wake.
Hiyo ni baada ya kupewa taarifa za kutimuliwa na uongozi wa timu hiyo kufuatia kipigo cha mabao 2-0 walichokipata dhidi ya Simba katika mechi ya Nani Mtani Jembe iliyochezwa wikiendi iliyopita.
Maximo alifika mazoezini hapo saa 2:35 akiwa na msaidizi wake, Leonardo Neiva, kiungo mkabaji wa timu hiyo raia wa Brazili, Emerson De Oliviera, ambao wote wamesitishiwa mikataba yao kwa ajili ya kuwaaga na Andrey Coutinho ambaye aliachwa kuendelea na mazoezi huku hao wengine wakiondoka.
Mbrazili huyo, aliwaaga wachezaji hao, zoezi lililotumia dakika kumi kwenye Uwanja wa Loyola, Mabibo jijini Dar es Salaam kabla ya kuondoka na gari ndogo aina ya Toyota Hiace kuelekea hotelini alipokwenda kufanya mazungumzo na viongozi wa timu hiyo.
Kwa mujibu wa mmoja wa wachezaji wa timu hiyo, kocha huyo mara baada ya kufika uwanjani hapo, aliwaita wachezaji hao na kuzungumza nao mambo mbalimbali kuhusiana na timu.Chanzo hicho kilisema, katika mazungumzo yake aliwatakia kila la kheri wachezaji na viongozi aliowaacha, Shadrack Nsajigwa na Salvatory Edward katika kuipa mafanikio ya mataji ya ubingwa kwa kuanzia na Ligi Kuu Bara.
“Inasikitisha kiukweli kocha wetu kufukuzwa ghafla, wamemshtukiza, ilitakiwa wampe muda kidogo wa kuiandaa timu na siyo kumfukuza baada ya kufungwa na Simba katika Nani Mtani Jembe.
“Alifika leo asubuhi akiwa na msaidizi wake, Neiva, Emerson na Coutinho kwa ajili ya kutuaga wachezaji, baada ya kufika tukazungumza naye kama dakika kumi na baadaye akaingia kwenye gari na kuondoka na kumuacha Coutinho akiendelea na mazoezi.
“Aliongea maneno mengi, lakini kikubwa alitutia moyo wa kuendelea kufanya vizuri katika mechi za ligi kuu na kututaka kumpa ushirikiano kocha mpya atakayekuja kutufundisha,” alisema mchezaji huyo huku akionekana kuwa na majonzi.
Maximo ambaye ameiacha Yanga ikiwa katika nafasi ya pili kwenye ligi akiwa kwenye gari wakati anatoka kwenye lango la Loyola, alionekana kuwa na huzuni kubwa, huku akikuna kichwa.
+

Pluijm: Tulieni, nimekuja kazini

Kocha mpya wa Yanga, Hans van der Pluijm.
KOCHA mpya wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema yuko tayari kuanza kazi na Yanga na kuahidi, amani itarejea.
Pluijm raia wa Uholanzi aliwasili nchini saa 8:30 usiku akitokea Accra, Ghana, alisema hawezi kuzungumza mengi lakini anachoamini atafanya kazi kwa juhudi kwa kuwa Tanzania kwake ni nyumbani, anaujua ushindani wake.
“Bado sijakutana na uongozi wa Yanga, lakini najua nimekuja kwa ajili ya kazi. Tukikubaliana nitafanya kazi kwa juhudi na kuhakikisha amani inarejea.“Najua mashabiki wanataka kuona matokeo ya ushindi. Hivyo ni suala la subira kidogo,” alisema.
Kuhusiana na kutaka Kocha Charles Mkwasa awe msaidizi wake, Pluijm alisema ni mapema sana kulizungumzia suala hilo.“Siwezi kuzungumzia lolote, nasubiri nikikutana na uongozi, nitajua la kusema,” alisema Pluijm raia wa Uholanzi ambaye aliondoka Yanga kwenda kujiunga na Al Shaolah FC ya Oman.
Taarifa nyingine zinaeleza kocha huyo alitarajia kukutana na uongozi wa Yanga, jana au leo kumalizana nao.Yanga wameamua kumrejesha achukue nafasi ya Maximo ambaye anatarajia kuondoka ndani ya siku mbili kurejea kwao Brazil.
Yanga imeonekana kutoridhishwa na kazi ya Mbrazili huyo aliyewahi kuinoa Taifa Stars baada ya mechi saba tu za ligi. Anaiacha timu yake ikiwa katika nafasi ya pili nyumba ya Mtibwa Sugar.
+

Monday, 15 December 2014

16 BORA LIGI YA MABINGWA ULAYA;ARSENAL HATIMAYE YAWAKWEPA VIGOGO BAYERN NA BARCELONA




Ratiba ya mchuano wa hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa ulaya imetoka huku ikishuhudia timu kama Arsenal ikivikwepa vigogo kama Bayern Munich na Barcelona wakati ndugu zao Manchester City wakiumana na mmoja wa vigogo hivyo Barcelona,waingereza wengine Chelsea wenyewe wataumana na matajiri wa Ufaransa PSG ikiwa ni kumbukumbu ya robo fainali ya msimu uliopita.Mechi za raundi ya kwanza katika hatua hii zinatarajiwa kuchezwa kati ya tarehe 17 na 25 februari.
+

Saturday, 6 December 2014

RONALDO AFUNGA GOLI LA 200 KWENYE LA LIGA NA KUWEKA REKODI YA KUWA NA HATRICK NYINGI

'We need new words to describe Ronaldo'
Mshambuliaji huyu wa kireno jumamosi hii amefunga mabao matatu katika mechi dhidi ya celta vigo
na kuweza kufikisha hatrick nyingi zaidi katika la liga.
Ronaldo pia amefikisha goli lake la 200 baada ya kufunga mabao haya matatu dhidi ya celta.
Kabla ya mechi ya leo,aliingia uwanjani akiwa na mabao 197 katika mechi 177.Alifungua akaunti yake magoli kwa mkwaju mkali wa penati kabla ya mapumziko na kumalizia mengine mawili katika kipindi cha mwisho.
Sio kwamba kafikisha idadi hiyo tu ya magoli bali pia kavunja rekodi ya kufunga hatrick nyingi zaidi 23 katika ligi hiyo ya Hispania.
Punde baada ya kuweka rekodi hiyo alipumzishwa huku akishangiliwa na mashabiki wa timu ya nyumbani.
Mwanasoka huyu bora wa dunia mwaka 2013 amefikisha mabao 23 katika mechi 13 tu msimu huu.
+