Wednesday, 17 December 2014

Leave a Comment

Pluijm: Tulieni, nimekuja kazini

Kocha mpya wa Yanga, Hans van der Pluijm.
KOCHA mpya wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema yuko tayari kuanza kazi na Yanga na kuahidi, amani itarejea.
Pluijm raia wa Uholanzi aliwasili nchini saa 8:30 usiku akitokea Accra, Ghana, alisema hawezi kuzungumza mengi lakini anachoamini atafanya kazi kwa juhudi kwa kuwa Tanzania kwake ni nyumbani, anaujua ushindani wake.
“Bado sijakutana na uongozi wa Yanga, lakini najua nimekuja kwa ajili ya kazi. Tukikubaliana nitafanya kazi kwa juhudi na kuhakikisha amani inarejea.“Najua mashabiki wanataka kuona matokeo ya ushindi. Hivyo ni suala la subira kidogo,” alisema.
Kuhusiana na kutaka Kocha Charles Mkwasa awe msaidizi wake, Pluijm alisema ni mapema sana kulizungumzia suala hilo.“Siwezi kuzungumzia lolote, nasubiri nikikutana na uongozi, nitajua la kusema,” alisema Pluijm raia wa Uholanzi ambaye aliondoka Yanga kwenda kujiunga na Al Shaolah FC ya Oman.
Taarifa nyingine zinaeleza kocha huyo alitarajia kukutana na uongozi wa Yanga, jana au leo kumalizana nao.Yanga wameamua kumrejesha achukue nafasi ya Maximo ambaye anatarajia kuondoka ndani ya siku mbili kurejea kwao Brazil.
Yanga imeonekana kutoridhishwa na kazi ya Mbrazili huyo aliyewahi kuinoa Taifa Stars baada ya mechi saba tu za ligi. Anaiacha timu yake ikiwa katika nafasi ya pili nyumba ya Mtibwa Sugar.

0 comments: