Monday, 29 December 2014

Leave a Comment

Makipa wanaolipwa zaidi: Casillas afunika ulaya

 
 
Soka ni mchezo unaopendwa sana ulimwenguni na wachezaji wengi wa mchezo huo kwenye ligi mbalimbali za Ulaya wamekuwa wakivuna fedha nyingi kutoka na mchezo huo.
Wachezaji wanaolipwa fedha nyingi ni wale wanaocheza nafasi za ushambuliaji au viungo washambuliaji. Kwa sababu Lionel Messi analipwa na klabu yake ya Barcelona Pauni 30 milioni kwa mwaka, Cristiano Ronaldo analipwa na Real Madrid Pauni 25.7 milioni kwa mwaka, Gareth Bale analipwa na Real Madrid Pauni 20.7 milioni, Neymar analipwa na klabu yake ya Barcelona Pauni 17.1 milioni kwa mwaka, Sergio Aguero analipwa na Manchester City Pauni 16.3 milioni kwa mwaka, Wayne Rooney analipwa na Manchester United Pauni 15.4 milioni kwa mwaka, Zlatan Ibrahimovic analipwa na PSG Pauni15 milioni kwa mwaka na Yaya Toure analipwa na Manchester City Pauni14.2 milioni.
Hata hivyo, hali ni tofauti kwa makipa kwani huwa hawalipwi fedha nyingi kwa mwaka kama ambavyo wanalipwa washambuliaji. Wafuatao ni makipa wanaoongoza kwa kulipwa fedha nyingi kuliko makipa wengine:
1-Iker Casillas
Kipa Iker Cassilas wa Real Madrid ndiye anayeshika nafasi ya kwanza kwa kulipwa mshahara mkubwa duniani kwani kwa mwaka analipwa Pauni 6.3 milioni.
2-Manuel Neuer
Kipa wa Bayern Munich, Manuel Neuer ndiye anayeshika nafasi ya pili kwa makipa wanaolipwa zaidi kwa sababu analipwa Pauni 5.6 milioni.
3-Petr Cech
Cech ni kati ya makipa bora katika Ligi Kuu ya England. Petr Cech analipwa na Chelsea mshahara wa Pauni 5.2 milioni kwa mwaka.
4-Joe Hart
Kipa wa Manchester City, Joe Hart ambaye amekuwa na misimu mizuri analipwa mshahara wa Pauni 4.68 milioni kwa mwaka.
5-Pepe Reina
 Kipa Pepe Reina wa Bayern Munich anashika nafasi ya tano kwa makipa wanaolipwa zaidi. Kiasi anacholipwa hivi sasa na Bayern ni Pauni 4.16 milioni kwa mwaka.
6-David De Gea
Kipa wa Manchester United, David De Gea hivi sasa yupo katika kiwango cha juu hivi sasa, klabu yake inamlipa mshahara wa Pauni 3.64 milioni kwa mwaka.
7-Hugo lloris
Kipa wa Tottenham, Hugo Lloris hivi sasa analipwa na klabu hiyo mshahara wa Pauni 3.59 milioni kwa mwaka.
8- Gianluigi Buffon
Kipa mzoefu wa Juventus, Gianluigi ‘Gigi’ Buffon anashika nafasi ya nane katika makipa wanaolipwa mishahara mikubwa. Buffon analipwa mshahara wa Pauni 3.17 milioni kwa mwaka.
9-Claudio Bravo
Kipa huyu wa klabu ya Barcelona analipwa na klabu hiyo Pauni 2.77 milioni kwa mwaka.
10-Salvatore Sirigu
Kipa anayefunga orodha ya makipa wanaolipwa fedha nyingi ni kipa wa Paris Saint Germain, Salvatore Sirigu. Kipa huyu analipwa mshahara wa Pauni 2.6 milioni kwa mwaka.

0 comments: