Mshambuliaji huyu wa kireno jumamosi hii amefunga mabao matatu katika mechi dhidi ya celta vigo
na kuweza kufikisha hatrick nyingi zaidi katika la liga.
Ronaldo pia amefikisha goli lake la 200 baada ya kufunga mabao haya matatu dhidi ya celta.
Kabla ya mechi ya leo,aliingia uwanjani akiwa na mabao 197 katika mechi 177.Alifungua akaunti yake magoli kwa mkwaju mkali wa penati kabla ya mapumziko na kumalizia mengine mawili katika kipindi cha mwisho.
Sio kwamba kafikisha idadi hiyo tu ya magoli bali pia kavunja rekodi ya kufunga hatrick nyingi zaidi 23 katika ligi hiyo ya Hispania.
Punde baada ya kuweka rekodi hiyo alipumzishwa huku akishangiliwa na mashabiki wa timu ya nyumbani.
Mwanasoka huyu bora wa dunia mwaka 2013 amefikisha mabao 23 katika mechi 13 tu msimu huu.
0 comments:
Post a Comment