Wema Sepetu, akiwashukuru mashabiki zake kwa sapoti waliyompa kwa mwaka 2014 na kumtambulisha msanii Luna.
Msanii
wa Bongo Fleva, Ally Luna (kushoto), akiimba wimbo wa kumsifia Wema
mara baada ya kutambulishwa kuwa chini ya Kampuni ya Endless Fame.
Msanii wa Bongo Fleva, Linex, akiimba huku shabiki yake akizungusha nyonga baada ya kuguswa na moja ya nyimbo zake.
Mmoja wa mabaunsa wa ukumbi huo akimuondoa jukwaani mrembo mmoja baada ya kuguswa na wimbo wa Mirra na kuamua kulivamia jukwaa.
Mtangazaji
wa Clouds FM, Soud Brown, akiwa na keki aliyopewa na Wema Sepetu kama
zawadi ya siku yake ya kuzaliwa ambayo ilifanyika usiku huo.
MKURUGENZI wa kampuni ya Endless Fame, Wema
Sepetu, usiku wa kuamkia leo amemtambulisha msanii mpya wa Bongo
Fleva, Ally Luna, ambaye takuwa mmoja wa wasanii wa kampuni hiyo na
kusimamiwa shughuli zote za kimuziki kama ilivyo kwa mwanamuziki Mirra.
Tukio hili lilifanyika ndani ya Ukumbi wa Club 71 uliopo Tegeta jijini Dar es Salaam ambapo kulikuwa pia na shoo maalum ya kufunga mwaka kwa kampuni hiyo na kuwashukuru wadau wote waliowaunga mkono.
Shoo hiyo ilisindikizwa na wasanii kibao wa Bongo Fleva, wakiwemo Bob Junior, Godzilah, Izzo Business, Barnaba Boy, Linex na Mirra.

0 comments:
Post a Comment