Wednesday, 17 December 2014

Leave a Comment

MAINDA AINGILIA TIMBWILI LA MDOGOWE



STAA wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’, Jumapili iliyopita alijikuta akigeuka baunsa wa kujitegemea na kuamulia ugomvi ambao unadaiwa kuwa chanzo chake ni mdogo wa mwigizaji huyo, Rose Peter ‘Muna’.
Mtangazaji wa Clouds TV, Castro Dickson.
Kwa mujibu wa chanzo makini, kwenye tukio hilo lililotokea katika Hoteli ya Lamada, Ilala jijini Dar, uliibuka ugomvi kati ya mwanamuziki wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Kalala Junior na mtangazaji wa Clouds TV, Castro Dickson ‘Mwananchi wa Kawaida’ wakimgombea Muna.
“Kulikuwa na sherehe ya mtoto wa mdogo wake Muna, Kalala ambaye ni mpenzi wa sasa wa Muna pamoja na Castro ambaye aliwahi kuwa x wa Muna huko nyuma, naye alialikwa, sasa walipokutana, mambo yakaharibika, shughuli ikawa pevu, wakataka kukunjana, ndipo Mainda akaingilia kati,” kilisema chanzo chetu.
Mdogo wake Mainda, Muna akiwa na Castro Dickson.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kwamba, ugomvi huo uliibuka mara baada ya Castro kuonekana akiteta chobingo na Muna ndipo Kalala ‘akamaindi’ na kuagiza mtu amuite ‘bebi’ wake huyo ili kumuondoa mikononi mwa Castro.
“Muna alitii amri ya bebi wake, akamfuata eneo alilokuwepo, huku nyuma uvumilivu ukamshinda Castro, akamfuata Muna katika eneo alilokuwepo na kuanza kurusha matusi ya nguoni kwa mbali, huku akimfuata Kalala ili ampige.
Mwanamuziki wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Kalala Junior.
“Bahati nzuri Mainda aliingilia na kumdaka mkono Castro kisha kumuondoa mahali hapo. Nimeshangaa kuona Mainda ana nguvu utafikiri mwanaume, kamtaiti Castro akamsindikiza kwenye gari lake, akatokomea kusikojulikana na kumuacha Muna akiteta na Kalala,” kilisema chanzo.
Hadi chanzo chetu kinaondoka eneo hilo, hali ilikuwa shwari hususan baada ya Castro kuondoka na bahati nzuri bethidei ilikuwa imeshafikia kikomo, waalikwa wote wakarudi makwao.

0 comments: