Wednesday, 17 December 2014

Leave a Comment

CHUCHU HANS ACHARUKA MADAI YA USALITI



KIMENUKA! Msanii wa filamu, Chuchu Hans ambaye ni mpenzi wa wa nguli wa filamu Bongo, Vicent Kigosi ‘Ray’, amecharuka ishu ya kumsaliti mpenzi wake huyo na jamaa anayedaiwa kuwa ni mfanyabiashara anayeishi maeneo ya Mbezi Beach Dar.
Msanii wa filamu, Chuchu Hans.
Chanzo kinasema pamoja na Chuchu kuwa na Ray kwa muda wote, lakini inadaiwa kuwa muda fulani amekuwa akitoka na kwenda Mbezi anapoishi kijana huyo.
Hata hivyo paparazi wetu aliamua kumvutia waya Chuchu na kuzungumza naye ishu hiyo ambapo alidai stori hizo zinasambazwa na watu ambao lengo ni kutaka kumchafua kwa mpenzi wake Ray.
“Watu hawapendi kuniona natoka na Ray na ni hao ndiyo wanaotumia muda mwingi kutaka kutuvuruga. Siwezi kufanya hivi na huyo jamaa sijui wa Mbezi kwanza simfahamu na pili jamii haitanielewa nikifanya hivi,” alisema Chuchu.

0 comments: