Staa huyo wa Ngoma ya Togola alinaswa na Ijumaa Wikienda ndani ya Club East 24 iliyopo Mikocheni jijini Dar, wikiendi iliyopita ambapo jamaa alikuwa bize akifanya yake bila kujali mashabiki waliokuwa wakimshangaa wakati B-Band chini ya Banana Zorro ikifanya makamuzi.
Wakati makamuzi ya bendi hiyo yakiwa yamepamba moto, Dully alionekana akikumbatiwa kimahaba na mrembo mmoja baada ya mwingine.
“Jamani yule si Dully ambaye amefiwa na baba yake juzi tu? Mbona amegandana na yule mrembo kule ukutani? Hebu waangalie wanafanya nini jamani? Duh! Kweli haya ni mambo ya kizungu,” alisikika mdada mmoja aliyeonekana kuwapiga chabo kwenye giza huku akimsisitiza mwenzake naye apige chabo.
Kufuatia tukio hilo, mwanahabari wetu alimfuata Dully kisha akampa pole na kumuuliza kulikoni kujivinjari klabu usiku huo uliokuwa ukielekea mishale ya saa nane na ushee?
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Dully alipokea pole kisha akamwaga utetezi wake:
“Nimetokea kwenye kikao cha kupanga hitima ya marehemu baba, nimeona nipitie hapa kupoza machungu ya msiba na kumsalimia swahiba wangu, Banana Zorro.”
Wadau waliokuwa ukumbini hapo walisema ni kawaida kwa mtu mwenye mawazo kujivinjari sehemu kama hiyo kupunguza mawazo na haina maana kujifungia ndani na kulia.
0 comments:
Post a Comment