Marehemu Sajuki alifariki dunia Januari 2.2013 , ambapo leo ametimiza miaka miwili, dua ya kumuombea ilianzia katika makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam ambapo marehemu Sajuki alizikwa na baadae kuhamia nyumbani kwake Tabata.
Akizungumza Wastara alisema anajisikia faraja sana kusoma dua kwa ajili ya mtu aliyempenda lakini pia anawashukuru wadau na wote waliojitokeza katika kufanikisha kisomo hicho.
Aidha wasanii mbalimbali wamejitokeza akiwemo Mohamed Mwikonge ‘’Frank’ Mtitu, Nisha, Bond na wengineo ambao pia wameomba na kuwakumbusha wasanii na wadau mbalimbali kuwakumbuka na kuwaenzi wasanii pindi wanapoaga dunia.
0 comments:
Post a Comment