Wednesday 31 December 2014

Leave a Comment

MILLEN MAGESE AMSAPRAIZ JOKATE

Mwanamitindo maarufu Bongo, ambaye anafanya kazi zake nje ya nchi Happyness Magesse ‘Millen’. Mwanamitindo maarufu Bongo, ambaye anafanya kazi zake nje ya nchi Happyness Magesse ‘Millen’ ambaye pia alishawahi kunyakua taji la Miss Tanzania 2001, ‘amemsapraiz’ mwanamitindo na mbunifu Jokate Mwegelo, kwa kumpatia keki yenye sura ya mdomo wake.
Awali, kulikuwa na kikao cha kawaida cha kujadili mambo mbalimbali ya kikazi baina yao kilichofanyika ndani ya hoteli ya Hyatt Kempisky, iliyopo Posta Jijini Dar, lakini kumbe Millen alikuwa ameandaa keki.
Mwanamitindo na mbunifu Jokate Mwegelo.
“Yaani mimi nilijua tunakutana kama tulivyopanga, lakini cha kushangaza nikakuta watu wakiongozwa na dada yangu Millen wameniandalia keki mbalimbali ikiwemo moja kama mdomo wangu kabisa na kidoti juu, kwa kweli nilifurahi sana siwezi kuelezea,” alisema Jokate.  

0 comments: