Monday, 15 December 2014

Leave a Comment

MTU MWENYE SILAHA AZIDI KUWASHIKILIA MATEKA KWENYE MGAHAWA JIJINI SYDNEY


Polisi wakimpokea mmoja wa mateka kutoka katika mgahawa wa Lindt jijini Sydney.
MTU mmoja mwenye silaha bado anaendelea kuwashikilia wafanyakazi na wateja katika mgahawa wa Lindt uliopo jijini Sydney nchini Australia.

Mateka ndani ya mgahawa huo wakiwa wameshika bendera yenye maandishi ya Kiarabu.
Baadhi ya watu ndani ya jengo hilo wameonekana kupitia madirisha wakiwa wamebeba bendera nyeusi zenye maneno ya Kiarabu.

Ulinzi mkali nje ya mgahawa.
Watu watano wameonekana wakikimbia kutoka katika jengo hilo la mgahawa japo mpaka sasa bado haijafahamika ni mateka wangapi wapo ndani.
Askari polisi waliozingira eneo lote la mgahawa huo wameeleza kuwa tayari wameanza kufanya mazungumzo na mtekaji huyo aliye ndani ya jengo.

Baadhi ya mitaa ikiwa imefungwa.
Mpaka sasa bado haijafahamika sababu za mtu huyo kuwateka watu ndani ya mgahawa huo.

0 comments: