Tuesday 30 December 2014

Leave a Comment

MAMA LWAKATARE HAFIKIRII KUGOMBEA UBUNGE MWAKANI



Mbunge wa Viti Maalum CCM ambaye pia ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God jijini Dar, Dk. Getrude Rwakatare (pichani) ameibuka na kusema hafikirii kugombea nafasi hiyo mwakani.Mbunge wa Viti Maalum CCM ambaye pia ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God jijini Dar, Dk. Getrude Rwakatare.
Akizungumza na gazeti hili juzi jijini Dar, Mama Rwakatare alisema amebaini kwenye siasa kuna watu wanataka kutumia nafasi hiyo kumchafua jambo ambalo linampa wakati mgumu ikizingatiwa kuwa ana watu wanaomwamini kiroho.
“Sifikirii kwa sasa kugombea ubunge mwakani, siasa ina mambo mengi sana, bora niendelee kumtumikia Mungu, kama wazo litanijia tena ni hapo baadaye,” alisema Mama Rwakatare.Mama Rwakatare ambaye pia ni mmiliki wa Shule za St. Mary’s alisema anaamini katika kumtumikia Mungu zaidi kuliko kujikita kwenye siasa.
Shule za St Mary’s zinazomilikiwa na Mchungaji Rwakatare zimekuwa juu kielimu karibu kila kona ya nchi.
Kwa mfano, Shule ya Sekondari ya St. Mary’s International iliyopo Mang’ula, Ifakara, Morogoro imekuwa ya kwanza kiwilaya, St. Mary’s International Kihonda Morogoro Mjini imekuwa ya pili kiwilaya na ya tano kimkoa na imetoa mwanafunzi bora Afrika Mashariki wa kwanza katika mashindano ya insha.
Bado shule za St. Mary’s ziliendelea kufanya vizuri kwani St. Mary’s Tabata jijini Dar ilikuwa ya sita kiwilaya na wanafunzi wote walichaguliwa kuendelea kidato cha tano.
Shule ya St. Mary’s Mbagala ilishika nafasi ya tano kiwilaya na wanafunzi wote wa darasa la saba walichaguliwa. Shule ya St. Mary’s Mbeya ilikuwa ya pili kiwilaya na ya sita kimkoa, mwaka jana ya kwanza kiwilaya na ya tatu kimkoa, watoto wote walichaguliwa.
Mkurugenzi wa shule hizo, Mama Rwakatare alisema shule zake zinafanya vizuri kutokana na kuwa na walimu wenye sifa.“Walimu wote wana sifa, ndiyo kigezo tunachosimamia ili kuajiri. Hii imetusaidia sana shule za St. Mary’s kuwa bora,” alisema mama Rwakatare.

0 comments: