Saturday, 13 December 2014

Leave a Comment

KIFO CHA MILIONEA MOSHI, USHIRIKINA WATAJWA

Upupu, Moshi
MWEZI mmoja baada ya mfanyabiashara wa Arusha, Timoth Mroki (36) kujiua kwa kujipiga risasi, mfanyabiashara milionea mwingine maarufu wa Moshi, Augustino Mallya (40), naye Jumatatu iliyopita alijiua kwa kujipiga risasi akiwa nyumbani kwake eneo la Karanga, mjini Moshi huku ushirikina ukitajwa.
Mfanyabiashara milionea maarufu wa Moshi, Augustino Mallya (40) aliyejiua kwa risasi.
Baadhi ya watu waliokuwa katika msiba huo walikuwa wakisikika wakisema kuwa msiba huo unaweza kuwa na mambo ya kishirikina kwa sababu vifo vya wafanyabiashara hao wawili mmoja akiwa na makazi Arusha, vinafanana na vina utata.
“Kuumwa siyo kifo, inawezekana wamechezewa na wabaya wao ndiyo maana wote wamejiua kwa risasi na kusababisha viongozi wa dini kushauri kwa kusema hili tuliangalie,” alisema muombolezaji mmoja kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini.
Milionea huyo alikuwa akijishughulisha na biashara za maduka ya bidhaa za jumla na nyumba za kupangisha katika eneo hilo la Karanga.
Milionea Augustino Mallya enzi za uhai wake.
Naye shemeji wa marehemu huyo, Peter Masawe alidai kuwa shemeji yake alijiua kwa kutumia bastola aina ya browing yenye namba 96682, na tukio hilo lilitokea siku moja kabla ya mfanyabiashara huyo hajatakiwa kusafiri kwenda India, ambako alikuwa akipatiwa matibabu ya tumbo kwa muda mrefu.
Tukio hilo lilithibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela ambaye alisema mke wa marehemu,  Elizabeth Mallya, ndiye aliyebaini tukio la mumewe kujiua kwa kujipiga risasi moja kifuani akiwa sebuleni kwake, ambapo alitoa taarifa polisi.

0 comments: