MTANGAZAJI
wa Redio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amesema siku zote anapokuwa
kwenye uhusiano wa kimapenzi akigundua mtu wake ana ‘date’ na mwanamke
mwingine, kamwe hatathubutu kugombea bwana ila atanawa mikono.Mtangazaji wa Redio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ akipozi.
Akiongea hivi karibuni Dida alisema, hakuna kitu
ambacho kwake anaona ni cha kipuuzi kama kugombea penzi, kwa kuwa mtu
anapokusaliti ni wazi upendo wake umehamia kwa mtu mwingine hivyo hawezi
kujing’ang’aniza.“Nawashangaa sana wasichana wanaokosa kazi ya kufanya kwa kuanza kuwagombea wanaume, wengine wanadundana hadi kutoana manundu, hivi nigombee bwana kwani wanaume wameisha? Mimi nikimkuta mtu wangu yupo na mtu mwingine wala sijishughulishi, nachukua hamsini zangu,” alisema Dida.
0 comments:
Post a Comment