MWANAMUZIKI Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz'
usiku wa kuamkia leo ametwaa tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kiume Afrika
Mashariki (Best Male Artist in East Africa) kutoka Tuzo za 2014 AFRIMA
zilizofanyika huko jijini Lagos nchini Nigeria.
Mwanadada Vanessa Mdee yeye ameshinda tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike Afrika Mashariki (Best Female Artist in East Africa).Tuzo ya Diamond imepokelewa na mwanamuziki Peter Msechu aliyekuwepo katika zoezi hilo la utoaji tuzo maana na yeye alikuwa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tuzo hizo.
0 comments:
Post a Comment