Sunday, 28 December 2014

Leave a Comment

DIAMOND NA ZARI WALIVYOTUA NCHINI BURUNDI

Diamond na Zari wakiwa 'close' wakati wa safari yao ya kuelekea Bujumbura.
Diamond, Zari na baunsa wa Diamond maarufu kwa jina la Mwarabu baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Bujumbura, Burundi jana.
Diamond na Zari wakipokelewa katika Uwanja wa ndege wa Bujumbura jana.
BAADA ya shoo kali aliyoidondosha Dar Live katika Sikukuu ya Krismasi, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' akiwa na mpenzi wake wa sasa, Zarinah Hassan 'Zari' jana walitua nchini Burundi tayari kwa shoo itakayofanyika leo.
Staa huyo leo atakuwa na shoo katika Uwanja wa St. August, Burundi. Baada ya shoo hiyo, Diamond atakuwa na shoo nyingine Mwaka Mpya nchini Rwanda ambapo Januari 8 atapiga shoo nyingine nchini Nigeria.
Staa huyo kuzidi kuonyesha kuwa ni mahiri katika muziki, jana amejinyakulia tuzo nyingine ya Mwanamuziki Bora wa Kiume Afrika Mashariki kutoka Tuzo za Afrima 2014 zilizotolewa jijini Lagos nchini Nigeria.
Mtandao huu unaendelea kumpongeza staa huyo kwa juhudi zake na kumtakia kila la kheri katika kazi yake.

0 comments: