.
Watu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na Jumuiya ya
Kimataifa haitasahau namna mwama mama Catherine Samba alivyorejesha
amani na mshikamano katika nchi hiyo.
Catherine aliyekuwa Meya wa Jiji la Bangui kuanzia
Mei mwaka 2013, alipata nafasi ya pekee ya kupendekezwa kushika wadhifa
wa urais wa mpito miezi minane baadaye na kisha kuapishwa Januari 23,
2014 siku 12 tangu kuachia ngazi wa Dtojidia.
Catherine aliyezaliwa Juni 26, 1954 alivunja
rekodi na kuweka historia kwa kuwa rais wa kwanza wa mpito kwa miezi 18
ambayo bado anaitumikia, lakini pia kuwa rais wa kwanza mwanamke katika
taifa hilo lililokuwa likipitia kipindi cha mpito kutokana na machafuko
makali.
Aliteuliwa kuwa Meya wa Jiji la Bangui, mji Mkuu
wa CAR chini ya Baraza la Mpito la Taifa (CNT) baada ya mgogoro
uliolikabili taifa hilo kwa karibu mwaka mmoja, kuanzia mwaka 2012.
Uteuzi wake ulikubaliwa na pande zote mbili ziliziokuwa zikipingana, upande wa Seleka na Anti-balaca.
Katika uteuzi huo, Catherine ambaye alikuwa
mwanasheria na mfanyabiashara kabla ya kuingia katika siasa alikubalika
pia na Rais Francois Hollande wa Ufaransa, ambaye alikuwa akitafuta
namna ya kumaliza mgogoro wa taifa hilo.
Hata hivyo, awali hakutarajiwa kupata nafasi hiyo
ya kuwa rais wa mpito, kwa kuwa kulikuwa na zaidi ya watu wanane
waliokuwa wakitajwa kufikiriwa kupewa nafasi hiyo, lakini walitakiwa
kuthibitisha kwamba hawana uhusiano na makundi hayo mawili, yaani Seleka
na Anti-balaka.
Suala la kwanza, mama huyo anaweka historia na
kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo na zaidi kwa kufanikiwa
kurejesha amani na utulivu kuelekea kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa
kufanyika mwakani.
Hotuba yake aliyoitoa kwa ujasiri baada ya
kuthibitishwa na bunge la nchi hiyo akiwataka wahusika kuweka chini zana
zao na kusitisha mapigano ilikuwa na matunda makubwa.
Hakusita kuugeukia upande wa pili wa Seleca ambao
kwa kuwa walikuwa ndio waathirika wakubwa, aliwataka waache woga na
kwamba hakuwa tayari kusikia tena mauaji ya watu wasio na hatia, kwa
kujipambanua kwamba ni rais wa watu wote bila kuwa na ubaguzi.
Wito wake wa kutaka mazungumzo baina ya pande
mbili zilizohusika kwenye mgogoro wa kisiasa uliitikiwa kikamilifu na
pande zote mbili, na japokuwa aliingia madarakani katika kipindi ambacho
hakikuwa na utawala wa sheria, aliweza kurejesha taifa hilo kwenye
mstari na kuepuka kile kilichohofiwa kutokea, mauaji makubwa ya kimbari
kama ilivyowahi kutokea Rwanda.
Chanzo cha machafuko
Machafuko katika nchi hiyo yalishika kasi baada ya Rais Michael Dtojodia kupindua Serikali na kuchukua madaraka.
Hatua hiyo ilivuruga amani ya taifa hilo na kuibua
mapambano baina ya makundi mawili yaliyokuwa na mitizamo ya kidini,
Seleka na Anti-Balaka kuingia katika machafuko yaliyolielekeza taifa
hilo kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Baada ya Djotodia aliyeingia madarakani Machi 24,
2013 kwa kumuondoa Rais Francois Bozize, kukubali kuachia madaraka
Januari 10 mwaka huu kutokana na shinikizo kali la ndani na Jumuiya ya
Kimataifa, alitoa nafasi ya kuibuka kwa mwanamama Catherine.
0 comments:
Post a Comment