- Siri imefichuka! Bwa’mdogo a.k.a Serengeti Boy kutoka Kundi la Makomando, Fredy Felix amesimulia namna alivyofaidi penzi la staa wa Bongo Movies, Jacqueline Walper Massawe ‘Wolper’.
Akizungumza na GlobalTV Online kwenye mahojiano maalum juzikati, dogo huyo alisema kuwa katika maisha yake ya kimapenzi hakuna mwanamke ambaye aliwahi kutoka naye na kujiachia kwa furaha kama ilivyo kwa Wolper.
“Kiukweli msichana pekee ambaye nimewahi kuwa naye katika mapenzi na kumpenda kwa dhati ni Wolper pekee.“Mara yangu ya kwanza kukutana naye ilikuwa kama ‘sapraiz’ vile (habari zinasema kwamba walikutana maeneo ya Kinondoni), alipoingia kwangu nashukuru naye alinipenda na kunifanyia kila nilichohitaji.
“Nampenda sana Wolper na kila siku nimekuwa nikiahidi kwamba huyo ndiye mwanamke pekee ambaye nitakuja kuishi naye hata kama ni uzeeni maana ninampenda kutoka moyoni.“Sidhani kama moyo wangu utampenda mwanamke mwingine kama nilivyompenda Wolper. Kiukweli niliinjoi sana penzi lake,” alisema Fredy huku akijutia kumwagana naye bila sababu ya msingi.
Alipotafutwa Wolper ili kupata undani wa ishu hiyo simu yake ilipokelewa na aliposomewa mashtaka yake alikaa kimya bila kujibu chochote. Hata hivyo jitihada za kumtafuta zinaendelea.
0 comments:
Post a Comment