Huyu ndiye mtekaji raia wa Iran, Haron Monis.
WATU watatu wameuawa akiwemo mtekaji raia wa Iran, Haron Monis
aliyekuwa ameteka watu kwa zaidi ya saa 16 katika mgahawa mmoja jijini
Sydney nchini Australia jana baada ya Makomando kuvamia eneo hilo. Watu
wanne akiwemo polisi wamejeruhiwa wakati wa zoezi la uokoaji.
Mmoja wa majeruhi akipatiwa huduma ya kwanza.
Mtekaji huyo alikuwa ameachiwa kwa dhamana kwa makosa mbalimbali
aliyokuwa ameshitakiwa nayo. Moja ya makosa yake ilikuwa kuwatumia barua
ya matusi wazazi wa wanajeshi wa Australia waliofariki wakiwa
wanalitumikia jeshi la taifa hilo nchini Iraq.Waziri Mkuu wa Australia, Tony Abbott alisema lilikuwa jambo la kushtua sana kwamba wananchi wasio na hatia kutekwa nyara na mtu ambaye alikuwa anashinikizwa kisiasa.
Makomando walifyatua risasi na kisha kuingia ndani ya mgahawa huo huku wakirusha magurunedi.
0 comments:
Post a Comment