Saturday, 13 December 2014

Leave a Comment

LULU AWATIKISA MAPEDESHEE BUKOBA

Stori:Cescon Lucky
Staa wa Filamu za Kibongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ hivi karibuni alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya mapedeshee wa Bukoba kumganda na kumzonga huku kila mmoja akitaka namba yake ya simu.
Staa wa Filamu za Kibongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ akisherehesha.
Lulu aliongozana na wasanii wengine akiwemo Kulwa Kikumba ‘Dude’ kwenye uzinduzi wa hoteli iitwayo Nalfin iliyozinduliwa juzikati wilayani Muleba ambapo staa huyo alionekana kuwaumiza vichwa wanaume wakware wenye fedha zao.
Upupu iliyokuwa eneo la tukio ilishuhudia hayo kutokana na jinsi Lulu alivyowatikisa mapedeshee hao, baada ya uzinduzi, wanaume walimzonga huku wengine wakitaka mawasiliano ambapo Dude alilazimika kumuokoa kwa kugeuka baunsa.
Elizabeth Michael ‘Lulu’ akifurahia jambo.
Lulu hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo ila Dude alipopatikana alisema: “Ni kweli alikuwa na wakati mgumu, si unajua tena! Nililazimika kugeuka baunsa wake maana walimzonga.”

0 comments: