“Habari mpya ni kwamba Diamond Platnumz atakuwa mgeni rasmi katika pati 
ya Zari All White Ciroc, najihisi niko sahihi kwa sababu sioni kama kuna
 ushindani wowote, huyu ni mtu wangu na itabaki kuwa hivyo,” 
            
Licha ya kumzidi miaka 10, Zari atangaza rasmi kuwa ni mtu wake wa karibu kwa sasa
Johannesburg/Dar. Baada ya kuukimbia ukweli kwa 
kipindi cha mwezi mmoja, mwanamuziki Diamond Platnumz amethibitisha kuwa
 na uhusiano baina yake na staa maarufu kutoka Uganda, Zari ‘The Boss 
Lady’ na kwamba atakuwa mgeni rasmi katika hafla yake ijulikanayo ‘Zari 
All White Ciroc’ itakayofanyika mwezi huu.
Nyota huyo aliyevunja rekodi kwa kunyakua tuzo 
tatu za Channel O Music Video Awards (ChoMVA) wikiendi iliyopita, 
amekuwa akijadiliwa katika mitandao ya Tanzania na nje ya nchi kwa 
kuonekana na wanawake tofauti kila wakati, hali inayowachanganya 
mashabiki wake.
Hata hivyo, Diamond hajasita kuelezea hisia zake 
za sasa na kwamba yupo tayari kuhudhuria hafla hiyo, inayotarajiwa 
kufanyika Desemba 18.
“Nitakuwapo katika hafla hiyo, ni lazima nimuunge 
mkono, mbona kuna wengi wanaunga mkono na watu hawasemi, kama wanavyokaa
 kimya kwa wengine na huku iwe vivyo hivyo,” alisema Diamond huku 
akishindwa kukiri moja kwa moja kwamba ana uhusiano na Zari, “waswahili 
wanasema A na B yote majibu.”
Kwa upande wa Zari ambaye ndiye aliyekuwa 
msindikizaji mkuu wa Diamond wakati wa utolewaji wa tuzo hizo, 
alitangaza rasmi kwamba nyota huyo ndiye atakayekuwa mgeni rasmi katika 
hafla yake.
“Habari mpya ni kwamba Diamond Platnumz atakuwa 
mgeni rasmi katika pati ya Zari All White Ciroc, najihisi niko sahihi 
kwa sababu sioni kama kuna ushindani wowote, huyu ni mtu wangu na 
itabaki kuwa hivyo,” alisema Zari.
Zari ni nani?
Jina lake halisi anajulikana kama Zarinah Hassan 
maarufu Zari. Alizaliwa Septemba 23, 1980 huko Jinja, Uganda, kati ya 
shule alizosoma ni pamoja na Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jinja. 
Alikwenda Kampala na baadaye jijini London ambako alipata Diploma ya 
Cosmetology.
Zari alianza kujishughulisha na masuala ya muziki 
akiwa shule ya msingi. Kwa kuungwa mkono na familia yake mwaka 2007, 
alirekodi wimbo wa kwanza Oliwange (Wewe ni Wangu), albamu hiyo ilimpa 
tuzo Channel O ikiwa video bora ya Afrika Mashariki. Tangu hapo alitoa 
vibao kadhaa.
Mwanamuziki huyo ambaye ana asili ya India, 
Burundi, Uganda na Somalia, mwaka 2009 alipata tuzo ya mwanamuziki bora 
wa kike, huku mwaka 2008 akishinda tuzo ya Channel O akiwa mwanamuziki 
bora Afrika Mashariki.
Usiyoyajua kuhusu Zari
Zarinah ni mwanamuziki anayeishi Afrika Kusini na mumewe Ivan Semwanga anayedaiwa kuwa ametengana naye kwa sasa. Ana watoto watatu aliozaa na mumewe huyo ambao ni Pinto, Didy na Quincy ambao nao pia wanaishi Afrika Kusini. Ni mjasiriamali na mfanyabishara maarufu na tajiri anayeuza zaidi vipodozi na nguo. Anamiliki magari ya bei ghali
Zarinah ni mwanamuziki anayeishi Afrika Kusini na mumewe Ivan Semwanga anayedaiwa kuwa ametengana naye kwa sasa. Ana watoto watatu aliozaa na mumewe huyo ambao ni Pinto, Didy na Quincy ambao nao pia wanaishi Afrika Kusini. Ni mjasiriamali na mfanyabishara maarufu na tajiri anayeuza zaidi vipodozi na nguo. Anamiliki magari ya bei ghali




0 comments:
Post a Comment