Monday, 2 March 2015

Leave a Comment

LINAH & RECHO WAFANYA MAMBO YA AIBU KWEUPEE

Estelina Sanga ‘Linah’ na shostito wake, Winfrida Josephate ‘Recho’ wakilishana keki kwa mdomo.
Hamnazo? Masistaduu wa Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’ na shostito wake, Winfrida Josephate ‘Recho’, wamefanya mambo ya aibu mbele ya kadamnasi.
Tukio hilo la aibu lililoshuhudiwa na Ijumaa Wikienda, lilijiri hivi karibuni usiku kwenye bwawa la kuogelea (swimming pool) ndani ya Hoteli ya Regency-Mikocheni jijini Dar ambapo kulikuwa na ‘bethidei’ ya Recho.Awali, mastaa hao walianza kwa kulishana keki kwa staili ya njiwa (kwa mdomo), jambo lililoibua minong’ono mahali hapo.
Winfrida Josephate ‘Recho’.
Kama haitoshi, baada ya tukio hilo, wawili hao waliweka mapozi tata wakipiga picha zilizowaonesha nusu utupu huku vinguo walivyovaa vikiacha wazi sehemu kubwa ya maumbile yao nyeti.
“Duh! Hawa watoto sasa ni too much, waone walivyojiachia na vivazi vya aibu, yaani hawatazamiki mara mbili,” alisikika mmoja wa wahudhuriaji wa pati hiyo.Baada ya kunasa tukio hilo, mwana-habari wetu aliwafuata wawili hao kutaka kujua kulikoni kujiachia kihasara-hasara ambapo waliomba waachwe wafanye yao

0 comments: