MSANII wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ambaye pia anafahamika kama Shishi Baby, amesema baadhi ya watu wana chuki naye kiasi kwamba wanatamani kumtoa roho kwa kutopenda mafanikio yake.
Akipiga stori mara baada ya ziara yake ya kimuziki barani Ulaya, Shishi Baby alisema katika mitandao ya kijamii, alizushiwa kuwa alienda huko akiwa na mwanaume badala ya ukweli kwamba alifuata shoo katika miji tofauti.
“Yaani watu wana roho mbaya sana, wanatamani nikiwa nimepanda ndege waitungue nife na ndiyo maana wanazusha, namuomba Mungu sana maana maadui wanazidi kila kukicha kisa maendeleo yangu tu,” alisema.
0 comments:
Post a Comment