LILE ndinga aina ya Nissan Murano alilozawadiwa supastaa Wema Sepetu na aliyekuwa mchumba wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’, limeanza kumchefua mrembo huyo kiasi cha kulisusa.
Ndinga aina ya Nissan Murano alilozawadiwa supastaa Wema Sepetu na aliyekuwa mchumba wake, Nasibu Abdul ‘Diamond'.
Tukio hilo lilijidhihirisha wazi juzikati
nyumbani kwa staa huyo, Kijitonyama jijini Dar, ambapo Wema alitamka
hadharani kuwa kwa sasa analichukia kupita maelezo gari hilo
alilozawadiwa na Diamond kwenye sherehe yake ya kuzaliwa.
Wema Sepetu akitafakari jambo.
“Bwana acha nitumie hili gari lingine kwenda airport hilo Murano
sitaki hata kulisikia, sijui najisikiaje hata nikiliona,” alisikika
Wema. “Siku hizi sipendi kutumia hili Murano tena nalichukia kweli, inafikia kipindi nakosa raha nikiliona lakini ukiniuliza sababu ya kulichukia kiasi hicho hata sina sijui nimezoea sana kutumia BMW, ndiyo maana najikuta nalichukia gari hili,” alisema Wema.
Nasibu Abdul ‘Diamond'akipozi.
Kwenye bethidei yake iliyofanyika Septemba, mwaka huu, Wema
alizawadiwa magari mawili. La kwanza lilikuwa ni BMW 545i (Sh. Milioni
56) ambalo liliibua utata juu ya mtu aliyemzawadia na la pili ni Nissan
Murano (Sh. milioni 36) alilopewa na Diamond.
0 comments:
Post a Comment