HUYO ni mrembo kutoka watu wa jamii ya Surma nchini Ethiopia ambayo inajumuisha makabila ya Suri, Mursi na Me’en. Bila shaka anavutia japokuwa anashitua kidogo! Jamii ya watu hao iko Kusini mwa nchi hiyo na ni wafugaji kama walivyo Wamasai nchini Tanzania.
Kwa kifupi, ili kupata urembo huo, mdomo wa chini wa mwanamke hutobolewa na kuwekwa kijiti kidogo, na unapopona huwekwa kijiti kikubwa zaidi na zaidi hadi kisahani kikubwa cha mbao kama kinavyoonekana.
Hivyo mdomo huzidi kupanuka zaidi na kuvutia zaidi. Huenda hufikia kiasi cha kutisha au kuogopesha – hii ni kwa mtazamaji asiyekuwa wa jamii ya Surma. Hili huenda sambamba na kung’olewa kwa meno mawili ya chini ili kuruhusu uwekaji wa visahani hivyo vya miti au udongo.
Urembo huo huanzishwa kwa msichana akifikia miaka 14 au 15 ambapo hufichwa mahali maalum na kufanyiwa hivyo. Mwenye mdomo mkubwa zaidi ndiye hupata mahari kubwa zaidi ya ng’ombe! Hivyo, wazazi hujitahidi kuipanua midomo ya mabinti zao kiasi iwezekanavyo.
Hata hivyo, historia inasema kwamba, ili kukwepa wanawake wao kuchukuliwa na wafanya biashara ya utumwa kutoka nje, midomo yao “ilivurugwa” hivyo ili wakamata watumwa wasiwe na hamu ya kuwachukua na kuwapeleka utumwani.
Ni utamaduni unaofurahisha, au siyo? Kwa vile tunaishi katika utandawazi, si vibaya kuujaribu utamaduni huo.
0 comments:
Post a Comment