

TUNAAMBIWA
kuwa kuishi vizuri ni pamoja na kula chakula bora na sahihi. Pia, mtu
anayeishi vizuri ni yule ambaye hasumbuliwi na maradhi hatari na njia
pekee ya kuulinda mwili dhidi ya maradhi hatari ni kujua ipasavyo na
kuvitumia vyakula bora pamoja na kufanya mazoezi.
Katika makala
yafuatayo, nitakuorodhoshea baadhi ya vyakula vinavyotajwa kuwa bora
(super foods) ambavyo faida zake mwilini vimeanishwa. Kwa mlaji,
linakuwa jambo la busara kujua faida ya kila chakula unachoingiza
tumboni. Kwa mujibu wa mwandishi wa makala kuhusu vyakula hivi bora,
Bw.Hakeem Rahman, hivi ni vyakula vinavyowafanya “wenye afya nzuri
kuendelea kuwa na afya nzuri zaidi na wenye afya mbovu, kuwa na afya
nzuri.”
SAMAKIWana virutubisho aina ya Omega 3
ambavyo huulinda moyo dhidi ya maradhi. Samaki pia wana virutubisho
vinavyomuongezea mlaji uwezo wa kukumbuka (memory), kuna virutubisho
vyenye uwezo wa kupambana na kansa mwilini, kuongeza kinga mwilini na
kuondoa mafuta mabaya mwilini (Bad cholesterol). (unashauriwa kula
samaki kwa wingi kadiri uwezavyo).
Baadhi ya virutubisho muhimu
vinavyopatikana kwenye samaki ni pamoja na vitamini D, vitamin 12,
vitamini B3, vitamini B6, Omega 3 Fatty acids, protini na madini
mengine mengi.
KARANGAUnaweza ukazidharau
karanga, lakini zina faida kubwa mwilini. Miongoni mwa faida zake ni
pamoja na kuimarisha afya ya moyo, hupunguza kolestro mbaya mwilini na
kuongeza kolestro nzuri. Mafuta mazuri yaliyomo kwenye karanga hupunguza
shinikizo la juu la damu na huponya magonjwa ya moyo na hupunguza
uzito. Faida zote hizi unaweza kuzipata kutoka kwenye karanga au siagi
iliyotengenezwa kutokana na karanga (peanut butter). (unashauriwa kula
kiasi kadhaa kila siku, hasa za kuchemsha ndiyo nzuri).
KAROTIMiongoni
mwa faida nyingi za karoti ni pamoja na kushusha kolestro mbaya
mwilini, kupunguza unene, kuimarisha nuru ya macho, kuimarisha shinikizo
la damu, inatoa kinga kwenye figo na inaimarisha sukari mwilini. (kula
kadiri unavyoweza, mbichi au zilizochemshwa).
MAHARAGE YA SOYAHaya
ni maharage bora kabisa ambayo yana faida nyingi mwilini, ikiwemo
kushusha shinikizo la damu, kuimarisha sukari mwilini, kupambana na
ugonjwa wa kisukari, figo, moyo, kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa kansa
ya kibofu na magonjwa mengine ya wanawake.
PAPAI, TIKITI MAJIMiongoni
mwa matunda muhimu mwilini ambayo hata mgonjwa wa kisukari anashauriwa
kuyala ni pamoja na papai na tikitimaji ambayo yanaelezwa kuwa na
kiwango kikubwa cha ufumwele (fibre) na hivyo kutoa mchango mkubwa sana
katika kuimarisha kiwango cha sukari mwilini. (kula kiasi cha moja
katika ya matunda hayo mawili, kila siku).
KITUNGUU SAUMUHiki
ni kiungo cha mboga, licha ya kuonekana kama ni kiungo cha kuongezea
ladha tu ya chakula, lakini ni miongoni mwa vyakula vyenye faida kubwa
katika afya zetu. Kitunguu saumu husaidia kuyeyusha damu mwilini hivyo
kumuepusha mlaji kushikwa na ugonjwa wa moyo pamoja na presha. Kitunguu
hicho pia hutoa kinga kwenye ini na huondoa maumivu ya viungo. Kula
angalau kitunguu kimoja mara moja kwa wiki.